HEADING ANIMATIONS

HEADING ANIMATIONS

FANYA KAZI YA MUNGU

FANYA KAZI YA MUNGU

Sunday, May 6, 2012

MTANGAZAJI WA PRAISE POWER RADIO, ERICK BRIGHTON AMVALISHA PETE MPENZI WAKE NDANI YA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B-
DAR ES SALAAM
Leo ni siku ambayo Erick Brighton hataisahau maishani mwake kwa kitendo cha ujasiri na kujidhihirisha kuwa sasa anaenda katika hatua nyingine ya kuwa na mke aliyedhibitishwa madhabahuni na mbele ya mchungaji wake Dr. Getrude Rwakatare.

Ilikuwa ni siku ya furaha, ndelemo na vifijo baada ya Erick kumvisha pete mchumba wake. Hii inaonyesha kuwa kila jambo lina wakati wake, kinachotakiwa ni kuwa na uvumilivu na kukaa katika maombi ili siku ya siku upate mchumba wa ukweli....

Ngoja tuone kilichotokea......

 Erick Brighton (wa tatu kutoka kulia) akifutia mchumba wake na Mchungaji Getrude Rwakatare
 Waumini wakishuhudia pete ikivishwa
 Mchungaji Lukumay wa pili kutoka kulia akifuatilia kile kinchozungumzwa na mchungaji Getrude Rwakatare

Mama mtarajiwa wa Erick Brighton akimuakikishia mchungaji wake kuwa mume aliyempata ni hakika na sio "copy"

 Marafiki wa maharusi watarajiwa wakiwa tayari kuwapokea 
 Maharusi watatarijiwa wakisikiliza neno kutoka kwa mchungaji wao
Pete ikivishwa

 Maombi yakiendelea
 Mchungaji Getrude Rwakatare akiwaombia maharusi watarajiwa

No kutembea, Erick akiwaamebebwa na rafiki zake---baada ya kutoka madhabahuni




 Blogger na meneja masoko wa Glorious Celebration, Rulea Sanga (kushoto) hakukosa katika tukio hili.
Kutoka kushoto ni Kisaka wa Praise Power Radio,  Bony wa Channel Ten, Erick na Kisaka mkubwa
 Hawa wote ni watangazaji wa Praise Power Radio na majina yao ni akina Erick na wanajiita mapacha ila kinachowatofautisha ni kwamba wa kulia ameoa na wa kushoto bado...maombi yanatakiwa kwa mtumishi huyu..hahahahah!!!! mtani
Lister mwenye nyekundu hakukosa katika tukio hili.

No comments:

Post a Comment